Pages

Subscribe:

Tuesday, 27 January 2015

Mbona mpaka sasa TFF imekaa kimya??



BEKI wa AC MILAN, Philippe Mexes amefungiwa michezo minne baada ya kumpiga nahodha wa LAZIO , Stefano Mauri wakati wa mchezo wa ligi kuu ya SEREA A.




MEXES ni mchezaji wa kimataifa wa Ufaransa na alitolewa kwa kadi nyekundu na hiyo kadi nyekundi ni ya 16 kupewa mchezaji huyo tangu alipoanza kucheza soka.



Tukio kama hilo linafanana na lile lililotokea hapa nchini siku chache zilizopita kwa mchezaji AMIS TABWE kupigwa na beki wa RUVU SHOOTING.

Mbona mpaka sasa TFF imekaa kimya??

Manny Pacquiao vs Floyd Mayweather



WAKATI Mashabiki wa ngumi Ulimwenguni wakitaka mabondia mashuhuri ulimwenguni Manny Pacquiao
apambane na bondia Floyd Mayweather mwaka huu , kila mmoja yaani mabondia hao wamekuwa katika shughuli tofauti za kijamii.

Manny Pacquiao
MISS UNIVERSE
Mfano bondia Manny Pacquiao alikuwa katika shughuli ya kuwa jaji wiki hii katika shindano la MISS UNIVERSE ambapo mrembo kutoka COLOMBIA PAULINA VEGA aliibuka mshindi katika shindano hilo ambalo TANZANIA iliwakilishwa na mrembo NALE BONIFACE.

MANNY kwa sasa ana utajiri wa kiasi cha dola milioni MIA TATU na katika shindano hilo alimuuliza swali mrembo kutoka Marekani NIA SANCHEZ.


 
Huku bondia FLOYD MAYWETHER akifuatilia kwa makini pambano la kikapu kati ya LOS ANGELES CLIPPERS ambayo ilikuwa ikicheza na BROOKLYN NETS katika pambano ambalo mashabiki walipaza sauti wakimwambia wanamtaka Manny Pacquiao.
FLOYD MAYWETHER
 

Monday, 26 January 2015

Etoo kucheza SEREA A



Samuel Eto’o kuichezea Sampdoria.
  • Amefanya vipimo.
  • Sampdoria ipo nafasi ya nne Serea A.


Mchezaji wa kimataifa kutoka Cameroon , Samwel Etoo amekamilisha taratibu za uhamisho kutoka Everton kwenda Sampdoria.



          Samwel Etoo
        kucheza Serie A



  Samwel Etoo
kucheza Serie A



  
           Samwel Etoo

        kucheza Serie A

BENDI YAMOTO

TIMU za EQUTORIAL GUINEA na CONGO BRAZAVILLE zimetinga robo fainali huku kocha wa E.Guinea , Esteban Becker akiwa ni mtu mwenye furaha baada ya kuifikisha timu hiyo hatua hiyo huku yeye akikabidhiwa timu siku 11 kabla ya kuanza kwa mashindano hayo.
Kocha wa E.Guinea , Esteban Becker

Sunday, 25 January 2015

EQUTORIAL GUINEA YAENDA ROBO FAINALI NA CONGO

TIMU za EQUTORIAL GUINEA na CONGO BRAZAVILLE zimetinga robo fainali huku kocha wa E.Guinea , Esteban Becker akiwa ni mtu mwenye furaha baada ya kuifikisha timu hiyo hatua hiyo huku yeye akikabidhiwa timu siku 11 kabla ya kuanza kwa mashindano hayo.
Kocha wa E.Guinea , Esteban Becker

Thursday, 22 January 2015

RAGE ATAKA FURSA KWA WACHEZAJI WA TANZANIA

KIONGOZI wa zamani wa klabu ya SIMBA na shirikisho la soka nchini TFF , ISMAIL ADEN RAGE amevitaka vilabu vya soka nchini kuwa na mipango endelevu hasa kwa wachezaji wa hapa nyumbani ili waweze kucheza nje ya nchi.

RAGE ameyasema hayo baada ya mshambuliaji wa TP MAZEMBE, MBWANA SAMATTA kupata fursa ya kwenda kufanya majaribio katika klabu kubwa ya RUSSIA ya CSKA MOSCOW.


MBWANA ni miongoni mwa wachezaji wanaofanyiwa majaribio na klabu hiyo ya CSKA MOSCOW ambayo hushiriki katika michuano mikubwa ya vilabu barani Ulaya.

Wakati akiwa mazoezini MBWANA aliumia enka na hivyo hakucheza mchezo kati ya CSKA MOSCOW na SION ya USWISI ambayo SION ilifungwa goli MOJA kwa BILA.


TAIFA STARS MABORESHO YATOKA SARE NA AMAVUBI


Kitoka Mwanza 

TIMU ya taifa ya maboresho ya TANZANIA imecheza mchezo wake wa kimataifa wa kirafiki na Amavumbi ya RWANDA kwenye uwanja wa CCM KIRUMBA MWANZA.

Kocha Mart Nooj
Katika mchezo huo dakika ya tisa RWANDA waliweza kupata goli kupitia kwa mchezaji JEAN BATISTA MUNGIRANEZA.

TAIFA STARS maboresho iliweza kusawazisha goli hilo katika dakika ya 43 ya mchezo kwa goli lililofungwa na FRIDAY KELVIN baada ya kupokea pasi kutoka kwa SIMON MSUVA.

Timu zote zinajiandaa na mashindano ya kombe la mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza timu za mataifa yao na ligi za nyumbani kwao yaani CHAN.


RWANDA ni mwenyeji wa mashindano ya CHAN yatakayofanyika mwakani, huku TANZANIA ikijiandaa na michezo ya kutafuta tiketi ya kucheza michuano hiyo.