YANGA YATAKA ADHABU SAKATA LA AMIS TAMBWE
TAMBWE- NIMEAMBIWA MANENO YA KIBAGUZI
KLABU ya
YANGA imeliomba shirikisho la soka nchini TFF kutoa uamuzi wa ugomvi
aliofanyiwa mchezaji wao AMIS TABWE wakati timu yao ilipocheza na RUVU SHOOTING
katika uwanja wa Taifa jijini DSM.
vurugu |
Mkuu wa
idara ya habari na mawasiliano JERRY MURO amesema vitendo kama hivyo
visipothibitiwa mapema italeta vuruge uwanjani.
Aidha
YANGA imeomba TFF ikague ripoti za waamuzi na makamisaa ili kufahamu na
kutokomeza vitendo vya fujo uwanjani kabla ya kutokea kwa vurugu kubwa.
AMISI
TAMBWE ambaye aliibuka mfungaji bora msimu uliopita akiwa na timu ya SIMBA
ameshangazwa na uchezaji wa kukabwa na akashutumu vikali maneno ya kibaguzi
yaliyotolewa na mchezaji wa RUVU SHOOTING, GEORGE MICHAEL kwamba ni mkimbizi.
Wachezaji hao wanne ambao Pluijm amesema wanafanyiwa fujo na
hujuma za waziwazi uwanjani ni Amissi Tambwe, Kpah Sherman na viungo wa pembeni
Andrey Coutinho na Simon Msuva.
Pluijm amesisitiza kwamba hataki timu yake ipendelewe na waamuzi, lakini akawaonya waamuzi hao kuhakikisha wanaongeza umakini kugundua rafu wanazochezewa washambuliaji wao ambao wamekuwa wakikamiwa vibaya na timu pinzani.
0 comments:
Post a Comment