Kitoka Mwanza
TIMU
ya taifa ya maboresho ya TANZANIA imecheza mchezo wake wa kimataifa wa kirafiki
na Amavumbi ya RWANDA kwenye uwanja wa CCM KIRUMBA MWANZA.
![]() |
Kocha Mart Nooj |
Katika
mchezo huo dakika ya tisa RWANDA waliweza kupata goli kupitia kwa mchezaji JEAN
BATISTA MUNGIRANEZA.
TAIFA
STARS maboresho iliweza kusawazisha goli hilo katika dakika ya 43 ya mchezo kwa
goli lililofungwa na FRIDAY KELVIN baada ya kupokea pasi kutoka kwa SIMON
MSUVA.
Timu
zote zinajiandaa na mashindano ya kombe la mataifa ya Afrika kwa wachezaji
wanaocheza timu za mataifa yao na ligi za nyumbani kwao yaani CHAN.
RWANDA
ni mwenyeji wa mashindano ya CHAN yatakayofanyika mwakani, huku TANZANIA
ikijiandaa na michezo ya kutafuta tiketi ya kucheza michuano hiyo.
0 comments:
Post a Comment