Afcon 2015: kocha wa Equatorial Guinea Becker akiri
udhaifu katika kikosi chake.
Kocha wa timu ya taifa ya Equatorial
Guinea , Esteban Becker anaamini kwamba kikosi chake kimekosa matayarisho ya
michuano ya AFCON baada ya kulazimishwa sare na CONGO BRAZAVILLE katika mchezo
wa ufunguzi.
Sare hiyo ni ya kufungana goli 1-1
na EQUTORIAL GUINEA iliweza kumiliki kukaa na goli iliyoipata mapema wakati wa
mchezo huo lakini katika dakika ya 87 goli hilo lilisawazishwa.
Kocha wa EQUTORIAL GUINEA, Esteban
Becker aliteuliwa kushika wadhifa wa kuwa kocha mkuu wa timu hiyo zikiwa
zimesalia siku 11 kuanza kwa fainali hizo.
0 comments:
Post a Comment