KIONGOZI
wa zamani wa klabu ya SIMBA na shirikisho la soka nchini TFF , ISMAIL ADEN RAGE
amevitaka vilabu vya soka nchini kuwa na mipango endelevu hasa kwa wachezaji wa
hapa nyumbani ili waweze kucheza nje ya nchi.
RAGE
ameyasema hayo baada ya mshambuliaji wa TP MAZEMBE, MBWANA SAMATTA kupata fursa
ya kwenda kufanya majaribio katika klabu kubwa ya RUSSIA ya CSKA MOSCOW.
MBWANA
ni miongoni mwa wachezaji wanaofanyiwa majaribio na klabu hiyo ya CSKA MOSCOW
ambayo hushiriki katika michuano mikubwa ya vilabu barani Ulaya.
Wakati
akiwa mazoezini MBWANA aliumia enka na hivyo hakucheza mchezo kati ya CSKA
MOSCOW na SION ya USWISI ambayo SION ilifungwa goli MOJA kwa BILA.
0 comments:
Post a Comment