Pages

Subscribe:

Saturday, 17 January 2015

AFCON bila NIGERIA

          AFCON bila SUPER EAGLES ni kichekesho

              IVORY COAST haina historia ya kunyakuwa kombe la AFCON
MICHUANO ya kombe la mataifa ya Afrika inaanza muda mchache huko EQUTORIAL GUINEA, lakini swali linakuja ni kwa vipi mabingwa wa AFRIKA NIGERIA hawakuweza kupata tiketi ya kucheza fainali hizo kubwa barani afrika.



Chipolopolo iliponyakuwa ubingwa 2012
SUPER EAGLES mwaka 2013 ilikuwa mabingwa wa afrika na mwaka 2014 ikapata tiketi ya kuwakilisha bara la Afrika kwenye mashindano ya kombe la dunia BRAZIL.
 
Ni vigumu kwa mtu yoyote kuamini kwamba NIGERIA haiku kwenye mashindano hayo ya EQUTORIAL GUINEA na je ni kutokana na mfumo wa mpira wa miguu barani Afrika au kuboreka kwa mpira wa Afrika?


Mwaka 1996, NIGERIA iliwahi kuingia majaribuni tena safari hii ikiwa ni kushindwa kushiriki fainali za kombe la mataifa ya Afrika kwa mwaka huo kutokana na Serikali ya nchi hiyo ilikuwa ikiongozwa kijeshi kukataa kupeka timu kwenye mashindano hayo.

Algeria inaingia katika michuano ya mwaka huu ikiwa inaongoza kwa ubora wa viwango Afrika kutokana na viwango vya ubora wa soka vinavyotolewa kila mwezi na FIFA.

Algeria ilifanikiwa kufika hatua ya 16 bora ya michuano ya kombe la dunia ya BRAZIL 2014.

Katika michezo ya kutafuta tiketi Algeria ama Desert Foxes waliweza kushinda michezo mitano kati ya sita na hivyo kumaliza wakiwa vinara katika mashindano hayo.

Algeria inawategemea wachezaji wake nyota Yacine Brahimi anayechezea PORTO, Sofiane Feghouli anayechezea Valencia na Islam Slimani wa Sporting Lisbon.

Pia ALGERIA ipo katika kundi la kifo pamoja na Ghana, Senegal na Afrika kusini katika mchezo wa kundi C. 

Timu nyingine inayopewa chapuo ni Burkina Faso ambayo haina historia nzuri ijapokuwa iliwahi kufika hatua ya fainali mwaka 2013 na kufungwa na SUPER EAGLES NIGERIA.

Zambia ilifanikiwa kunyakuwa kombe la AFCON mwaka 2013 kwa kuifunga IVORY COAST chini ya wakongwe Yaya Toure, Didier Drogba na Gervinho.

0 comments:

Post a Comment